August 27, 2026 12:22 pm
"Where Africa Comes to Stay Informed."
US Edition
Breaking
  • Central bank holds rates steady, signals two cuts before year end
  • Storm system strengthens off the coast, evacuation orders expand
  • Parliament passes landmark energy bill after overnight session
  • Tech index rebounds after early sell-off on chip earnings
  • Peace talks resume in Geneva as envoys return to the table
  • Central bank holds rates steady, signals two cuts before year end
Home / Business / AfDB: Nchi 22 za Afrika Zakabiliwa na Mzigo wa Madeni Huku Dola Bilioni 87 Zikienda Kulipa Riba
Business AfDB: Nchi 22 za Afrika Zakabiliwa na Mzigo wa Madeni Huku Dola Bilioni 87 Zikienda Kulipa Riba

AfDB: Nchi 22 za Afrika Zakabiliwa na Mzigo wa Madeni Huku Dola Bilioni 87 Zikienda Kulipa Riba

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeeleza kuwa kufikia Julai 2026, nchi 14 za Afrika zilikuwa katika hatari kubwa ya kuelemewa na madeni, huku nyingine nane tayari zikiwa zimeelemewa. Takwimu hizi zinaonyesha shinikizo linaloongezeka la mikopo ya serikali kwa uchumi wa bara hili.

Ripoti Mpya ya AfDB

Taarifa hizo zimo katika ripoti ya AfDB ya Novemba 2026 iitwayo Africa’s Macroeconomic Performance and Outlook, inayochambua hali ya deni la umma barani Afrika na udhaifu unaozidi kujitokeza.

Benki hiyo ilionya kuwa majukumu yanayoongezeka ya kulipa madeni yanazidi kubana nafasi ya kifedha ya serikali, na hivyo kupunguza uwezo wao wa kugharamia huduma muhimu na vipaumbele vya maendeleo.

Gharama ya Riba Yapanda

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuongezeka kwa utegemezi wa serikali za Afrika kwa mikopo ya kibiashara kutoka nje na mikopo ya ndani kumepandisha gharama za kulipa madeni na kuongeza hatari za kiuchumi.

Ripoti ilibainisha kuwa takriban dola bilioni 87 za Marekani ziliondoka barani Afrika kama gharama za riba kati ya mwaka 2022 na 2024, kiasi sawa na asilimia 19 ya malipo yote ya madeni. Katika mwaka 2024 pekee, riba ya madeni ya nje ilichukua asilimia 6.3 ya mapato ya serikali.

Aidha, sehemu ya mapato ya serikali inayotumika kulipa madeni ya nje iliongezeka kutoka asilimia 23.7 mwaka 2017 hadi asilimia 31 mwaka 2024, ishara ya mzigo unaozidi kuongezeka wa kulipa madeni ya kigeni.

Riba Zaidi Kuliko Afya

AfDB ilieleza kuwa gharama kubwa za madeni zinahamisha rasilimali kutoka kwenye matumizi muhimu ya afya, elimu na miundombinu. Kati ya mwaka 2021 na 2023, nchi 25 kati ya 51 za Afrika zenye takwimu zilizopo zilitumia fedha nyingi zaidi kulipa riba kuliko kugharamia huduma za afya.

Mabadiliko ya Vyanzo vya Mikopo

Benki hiyo ilitaja mabadiliko ya muundo wa deni la umma kama chanzo kingine cha hatari. Ilieleza kuwa nchi za Afrika zinazidi kuachana na mikopo ya masharti nafuu (concessional financing) na kugeukia wakopeshaji wasio wanachama wa Paris Club pamoja na vyanzo visivyo vya masharti nafuu, zikiwemo hati fungani za Eurobond, mikopo ya benki za kibiashara na mikopo ya pamoja (syndicated facilities).

Iliongeza kuwa nchi kadhaa pia zimegeukia mikopo ya ndani ili kukabiliana na shinikizo la matumizi linaloongezeka, ukusanyaji dhaifu wa mapato ya ndani na kupungua kwa fursa za kupata ufadhili wa kimataifa.

Matarajio na Hatari Zilizopo

Licha ya hatari hizo kuongezeka, AfDB inatabiri kuwa uwiano wa deni la umma kwa Pato la Taifa (GDP) barani Afrika utashuka kutoka wastani wa asilimia 62.6 mwaka 2025 hadi asilimia 60.7 ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo, benki hiyo ilitahadharisha kuwa matarajio hayo bado yako hatarini kutokana na uwezekano wa kudorora kwa ukuaji wa uchumi, kupanda zaidi kwa viwango vya riba, na kurejea kwa matumizi holela ya fedha za umma, hasa katika mikopo ya kibiashara.

Wito wa Usimamizi Bora wa Madeni

AfDB ilitoa wito wa kuimarishwa kwa usimamizi wa madeni, matumizi yenye tija zaidi ya fedha zinazokopwa, na nafuu ya madeni kwa wakati kwa nchi ambazo tayari zimeelemewa.

Benki hiyo ilieleza kuwa tangu mwaka 2020, nchi sita za Afrika zimepanga upya madeni yao ili kurejesha nafasi ya kifedha na kupata nafuu, ingawa ilisema maendeleo chini ya mfumo wa G20 Common Framework kwa ujumla yamekuwa ya polepole.

Business
0 0

Comments

0

Comments from guests are reviewed before they appear.

No comments yet. Be the first to share your thoughts.
Lang
Powered by Google
Customer Support

Hello! 👋 Welcome to Zone Yetu customer support. How can we assist you today?

Now
Powered by AI • Average response time: <1s