Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameshinda kesi mahakamani siku ya Jumatano, baada ya mahakama kuifuta ripoti ya jopo iliyodai kuwa huenda alikiuka katiba kuhusiana na tuhuma za utovu wa nidhamu zilizotokana na kashfa ya “Farmgate.”
Mahakama Kuu ya Western Cape ilitangaza kuwa matokeo ya jopo huru la bunge hayakuwa halali, na ikayaweka kando kabisa.
Akisoma uamuzi uliofikiwa kwa kauli moja na majaji wote, Jaji Nolwazi Mabindla-Boqwana alisema: “Kwa kuhitimisha, mahakama imebaini kuwa jopo (la bunge) lilielewa vibaya kimsingi majukumu yake.”
Mwaka 2022, jopo hilo lilihitimisha kuwa kulikuwa na ushahidi wa awali (prima facie) unaomtaka rais kujibu tuhuma dhidi yake, na kwamba huenda alikiuka katiba.
Kashfa hiyo inahusu wizi wa mafungu ya fedha taslimu yaliyokuwa yamefichwa ndani ya sofa katika shamba la Ramaphosa mwaka 2020.
Uamuzi huo ni ushindi mkubwa kwa rais, kwani unaondoa hitimisho muhimu lililokuwa likitishia kufufua upya uchunguzi kuhusu mwenendo wake katika sakata hilo.
Comments
0