August 27, 2026 12:22 pm
"Where Africa Comes to Stay Informed."
US Edition
Breaking
  • Central bank holds rates steady, signals two cuts before year end
  • Storm system strengthens off the coast, evacuation orders expand
  • Parliament passes landmark energy bill after overnight session
  • Tech index rebounds after early sell-off on chip earnings
  • Peace talks resume in Geneva as envoys return to the table
  • Central bank holds rates steady, signals two cuts before year end
Home / Health / Barrick Yasimamisha kwa Muda Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi Wake wa DRC kwa Hofu ya Ebola
Health Barrick Yasimamisha kwa Muda Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi Wake wa DRC kwa Hofu ya Ebola

Barrick Yasimamisha kwa Muda Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi Wake wa DRC kwa Hofu ya Ebola

Kampuni ya madini ya Canada, Barrick, imesema inawasimamisha kazi kwa muda wafanyakazi wasio wa lazima na kuimarisha uchunguzi wa kiafya, baada ya wagonjwa wawili wa Ebola kuthibitishwa karibu na mgodi wake wa dhahabu wa Kibali, kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Visa Viwili Vilivyosababisha Vifo

Ripoti zilizotolewa wiki iliyopita zilionyesha kuwa, kupitia memo ya ndani, Barrick ilieleza kuwa inawasimamisha kwa muda baadhi ya wafanyakazi na wakandarasi wadogo katika mgodi wa Kibali, baada ya mamlaka za afya kuthibitisha visa hivyo viwili, ambavyo vyote vilisababisha vifo.

Hakuna Mfanyakazi Aliyekutana na Wagonjwa

Katika majibu yake kwa barua pepe yaliyothibitisha ripoti hiyo, Barrick ilisema kuwa baada ya zoezi la kuwafuatilia watu waliokutana na wagonjwa, lililofanywa kwa ushirikiano na mamlaka za afya pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), hakuna mfanyakazi wala mkandarasi aliyebainika kuwa alikutana na wagonjwa hao.

Shughuli za Mgodi Zaendelea Kama Kawaida

Kampuni hiyo haikuweka wazi idadi ya wafanyakazi inaowa “kuwaondoa kazini kwa muda”, lakini ilisema shughuli katika mgodi huo zinaendelea kama kawaida.

Barrick ilikuwa tayari imetangaza mwezi Mei uliopita kuwa imeongeza tahadhari dhidi ya Ebola katika mgodi wa dhahabu wa Kibali, ulioko katika jimbo la Haut-Uele.

Umiliki wa Mgodi wa Kibali

Kibali, mmoja wa migodi mikubwa zaidi ya dhahabu barani Afrika, unamilikiwa kwa pamoja na Barrick na AngloGold Ashanti, kila moja ikiwa na hisa za asilimia 45, huku kampuni ya madini ya serikali ya Kongo, SOKIMO, ikimiliki asilimia 10 iliyobaki.

Mlipuko wa Pili kwa Ukubwa Kuwahi Kurekodiwa

Kwa mujibu wa takwimu za serikali, mlipuko wa Ebola nchini Kongo, ambao ni wa pili kwa ukubwa kuwahi kurekodiwa, umewaambukiza zaidi ya watu 11,000 na kuua zaidi ya watu 5,000.

Ingawa hakuna kisa cha Ebola kilichoripotiwa katika migodi mikubwa ya viwanda, mlipuko huo umeathiri shughuli za wachimbaji wadogo (artisanal mining).

Health
0 0

Comments

0

Comments from guests are reviewed before they appear.

No comments yet. Be the first to share your thoughts.
Lang
Powered by Google
Customer Support

Hello! 👋 Welcome to Zone Yetu customer support. How can we assist you today?

Now
Powered by AI • Average response time: <1s