Eni, kampuni ya nishati inayomilikiwa na serikali ya Italia, imetangaza Jumanne kuwa itaongeza uwezo wake wa kusindika gesi katika Jangwa la Magharibi nchini Misri kupitia mradi wake wa Meleiha Awamu ya Pili.
Kampuni hiyo ilisema imeanzisha shughuli za awali za uendelezaji wa kituo kipya cha gesi ndani ya eneo la leseni ya Merged Meleiha. Mradi huo utaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kusindika gesi na kuchangia ukuaji wa uzalishaji wa gesi nchini Misri, kampuni hiyo ilisema.
Kiwanda kipya kimeundwa kusindika hadi futi za ujazo milioni 100 za gesi kwa siku. Kitahakikisha muunganiko wa uzalishaji mpya na miundombinu iliyopo ya gesi nchini Misri, huku pia kikichangia kuongeza upatikanaji wa gesi kwa soko la ndani.
Kwa sasa, Eni ndiyo mzalishaji mkuu wa nishati nchini Misri, ikiwa na uzalishaji wa mafuta na gesi (hydrocarbon) wa takriban mapipa 242,000 kwa siku kwa kipimo cha usawa wa mafuta (oil equivalent) mwaka 2025.
Comments
0