Senegal: Maandamano ya kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais yaahirishwa

Nchini Senegali, zaidi ya wiki moja baada ya uamuzi wa kuahirisha uchaguzi wa rais kutoka Februari 25 hadi Desemba 15, 2024, mzozo kati ya mamlaka na wapinzani kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi unaendelea. Wakati maandamano makubwa yalipangwa na mashirika ya kiraia kufanyika Februari 12 huko Dakar, gavana wa mji mkuu alipiga marufuku maandamano hayo, na kushinikiza waandaaji kuahirisha maandamano haya dhidi ya kuahirishwa kwa kura kwa dakika za mwisho na rais kuongezwa muhula.

Add a Comment

Your email address will not be published.