Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) linadaiwa kulipa kimyakimya mamilioni ya dola za kodi alizokuwa akidaiwa rais wake, Gianni Infantino, nchini Marekani kwa miaka mitatu mfululizo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Ufaransa, Le Monde.
Inaripotiwa kuwa nyaraka za siri zilizopitiwa na gazeti hilo zinaonyesha kwamba FIFA ililipia majukumu ya kodi ya Infantino kwa miaka ya 2024, 2025 na 2026.
Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa rais huyo wa FIFA alinufaika na kanuni za ndani zenye unafuu wa kipekee, ambazo zililiruhusu shirikisho hilo kulipa bili zake za kodi.
Ripoti hiyo haikutaja kiasi kamili cha fedha ambacho FIFA ililipa kwa niaba ya Infantino. Hata hivyo, taarifa hizi zinaibua maswali kuhusu mipango ya kifedha ya ndani ya FIFA na manufaa anayopewa rais wake.
Comments
0