Manchester United imemfuta kazi kocha mkuu Michael Carrick, wakati klabu hiyo ikiwa ndani ya eneo la kushuka daraja kwenye Ligi Kuu ya England.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mmiliki Sir Jim Ratcliffe kukutana na viongozi wa klabu, Omar Berrada na Jason Wilcox, mjini Monaco.
Aliyekuwa kocha wa Tottenham na Chelsea, Mauricio Pochettino, anaripotiwa kuwa “yuko tayari kukubali ofa” ya kuchukua nafasi ya Carrick, huku United ikiwa tayari “imefungua mazungumzo” naye.
Uamuzi huo umekuja kufuatia sare ya mabao 4-4 dhidi ya Aston Villa siku ya Jumapili, matokeo yaliyoiacha United ikiendelea kubaki katika eneo la kushuka daraja.
Mashetani Wekundu wameshinda mechi moja tu kati ya 10 za mwanzo za ligi msimu huu.
Carrick alichukua usukani kama kocha wa muda mwezi Januari na kuiongoza klabu hadi kumaliza katika nafasi ya tatu, kabla ya kusaini mkataba wa miaka miwili wakati wa majira ya joto.
Comments
0