Kampuni ya mawasiliano ya Afrika Kusini, MTN Group, imetangaza Jumatatu kuwa mapato yake ya huduma yaliongezeka kwa zaidi ya asilimia 17 katika kipindi cha miezi tisa hadi Septemba 30, kwa kipimo cha sarafu isiyobadilika (constant currency).
Ukuaji huo ulisukumwa zaidi na kuimarika kwa biashara ya kampuni hiyo nchini Nigeria, pamoja na utendaji mzuri unaoendelea kushuhudiwa nchini Ghana.
MTN, ambayo ndiyo kampuni kubwa zaidi ya mawasiliano barani Afrika, ilieleza kuwa mapato yake ya huduma katika robo ya tatu ya mwaka yalipanda kwa asilimia 16.6.
Katika miezi tisa iliyoishia Septemba 30, mapato ya huduma ya kundi zima yalifikia randi bilioni 176.2 (takriban dola bilioni 10.68 za Marekani, kwa kiwango cha dola 1 = randi 16.49).
Kampuni hiyo imekuwa ikifuatilia uwezekano wa kupata leseni za benki katika baadhi ya masoko yake, kwa lengo la kupanua utoaji wa mikopo kwa kutumia fedha zake yenyewe.
MTN ilisema inatarajia ukuaji wa mapato ya huduma zake za kifedha kwa njia ya teknolojia (fintech) kwa mwaka mzima wa 2026 kubaki chini ya kiwango cha malengo yake ya muda wa kati. Hali hiyo imetokana na kuvurugika kwa huduma yake ya Airtime Advance nchini Nigeria.
Hata hivyo, kampuni hiyo ina matumaini kuwa huduma ya Airtime Advance itarejea katika viwango ilivyokuwa kabla ya kusimamishwa ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Comments
0